Saturday, 3 February 2018

WASTARA KWENDA INDIA KWA MATIBABU KESHO

Wastara Juma

BAADA ya gazeti hili kuandika habari yake kwa mara ya kwanza akiomba msaada wa matibabu ya mguu wake, hatimaye staa wa filamu Bongo, Wastara Juma amekamilisha kiasi cha shilingi milioni 37 alizokuwa akihitaji na kesho (Jumapili) anatarajia kuondoka nchini kuelekea kwenye Hospitali ya Sefaree iliyopo India kwa matibabu.

Wastara alisema kuwa, hakutarajia muitikio mkubwa wa kuchangiwa fedha hizo na anawashukuru wote waliofanikisha kupatikana kwa msaada huo.

“Niwashukuru Watanzania wote kwa kunichangia, nimshukuru Rais Magufuli na mkewe mama Janeth lakini kwa kipekee kabisa naomba nilishukuru gazeti lenu (Risasi Jumamosi) kwa kuwafanya watu wengine wajue nina tatizo gani na nahitaji msaada, bila nyie huenda mpaka leo ningekuwa nalia kitandani, asanteni na Mungu awabariki,” alisema Wastara.

Mbali na kulishukuru gazeti hili, Wastara pia ameishukuru Global TV Online ambayo ilirusha sauti yake na video ikionesha jinsi alivyokuwa akipata maumivu.


Chanzo - MuungwanaBlog

No comments:

Post a Comment