Sunday, 11 February 2018

Wagonjwa wanusurika kuteketea kwa moto


Wagonjwa waliokuwa wamelazwa katika hospitali ya mision ya Tenweek wamelazimika kuzikimbia wodi ili kuokoa maisha yao, baada ya jengo la hospitali hiyo kuwaka moto na kuteketeza baadhi ya majengo.


Hospitali hiyo ambayo ipo katika kaunti Bomet nchini Kenya, ilishika moto mara baada ya jiko la hospitali hiyo kulipuka na kuteketeza maeneo ya karibu ikiwemo store ya chakula na mgahawa, ambayo yako karibu na kitengo cha wagonjwa mahututi na wodi kuu.
Hata hivyo, Mkuu wa Polisi wa Kaunti hiyo, Samson Rukunga amesema kuwa jeshi la polisi lilijitahidi na kufanikiwa kuuzima moto huo ambapo hakuna madhara yeyote ya kibinadamu yaliyotokea.
Chanzo - Dar24

No comments:

Post a Comment