Friday, 9 February 2018

Mbasha ahairisha kuoa tena


STAA wa Muziki wa Injili, Emmanuel Mbasha ametoa kali ya mwaka baada ya kusema kuwa ameamua kuahirisha suala la kuoa tena na katika maisha yake ataishi kama ‘Yesu’ au Paulo kwani wote hao hawakuoa.

Akistorisha na Star Mix, Mbasha alisema licha ya kwamba ni mwanaume aliyekamilika lakini amekuwa akimuomba Mungu na kweli anamsaidia katika kushinda vishawishi vya shetani.

“Ukiona niko na mwanamke ujue ni rafiki wa kawaida tu, tangu niachane na mke (Flora Mbasha) sijawahi kuzini na niko kawaida tu sina matatizo yoyote, yote hiyo ni Mungu ananisaidia pamoja na kufanya mazoezi sana, sina mpenzi wala mchumba kama wengi wanavyozusha maneno ya uongo,” alisema Mbasha.


Emmanuel Mbasha akiwa na anayedaiwa kuwa mpenzi wake.

No comments:

Post a Comment