Thursday, 8 February 2018

MASHUA MBILI ZAZAMA NA KUUA WATU


Mashua mbili za abiria zimezama na kusababisha vifo vya watu sita huku wengine 12 hawajulikani walipo.


Hayo yametokea nchini Nigeria, kituo cha habari cha Nigeria Nan kimeripoti kuwa mashua hizo zilibeba watu 78 katika jimbo la Kebbe.
Mpaka sasa ni abiria 60 wameokolewa wakiwa salama, huku jitihada za kuwatafuta watu 12 waliopotea bado zikiwa zinaendelea.
Gavana mkuu wa Kebbe, Abubakar Dakingari ametaja chanzo cha ajali hiyo na kusema kuwa mashua hiyo ilibeba abiria wengi na mizigo mizto kuzidi uwezo wake.
Chanzo - Dar24

No comments:

Post a Comment