Sunday, 18 February 2018

Mama Salma Kikwete amewataka akina baba kuacha kutelekeza Familia zao

Mgeni rasmi wa tamasha la Mchizi Wangu 2018 Mama Salma Kikwete akikabidhi hati maalum kwa ‘Single Mothers’ wote ambayo itatumika kama sehemu ya utambuzi na kuyafanyia kazi mahitaji yao.

Mke wa rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma Kikwete amewataka akina baba kuacha kutelekeza familia zao pamoja na watoto na kuwaachia akina mama majukumu ya kuijenga familia.

Mama Salma ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum, alikuwa Mgeni rasmi kwenye Tamasha la Mchizi Wangu 2018 iliyoandaliwa maalum na EFM na ETV kwaajili ya kuwapa support ‘Single Mothers’.

Akiongea na Single Mothers waliojitokeza katika halfa hiyo ya kuwatia moyo iliyofanyika katika hoteli ya Golden Tulip, Mama Salma Kikwete alisema huu ni wakati sahihi wa ‘Single Mothers’ na kuamka na kuanza kufanya kazi kwa bidii ili kuinusuru familia yake.

“Nimeelezwa kuwa tamasha la leo linawaleta pamoja wanawake mbalimbali kutoka jiji la Daresalaam shabaha kuu ikiwa ni kuwawezesha wanawake, Hakuna badala ya mama, awe na mapungufu ya viungo ni mama, hata awe masikini ni mama yako, kwa kuwa umekaa kwenye tumbo lake mama si mdogo,” alisema Mama Salma Kikwete.

Aliongeza “Ni faraja kubwa kwangu kujumuika na wanawake wenzagu katika harakati za kumuinua mwanamke hili ni jambo ambalo mimi na wanawake wenzangu wa Taasisi ya WAMA tumekuwa tukiilifanya na napenda kuwahakikishia kuwa hatutaacha kulifanya,
wajibu wa mzazi kwa mototo ni wa kudumu haupaswi kuishia tu pale wanapotengana na wenza wao. Mtoto hana hatia.” Mama Salma Kikwete.

Naye Martha Mlata Mbunge wa viti maalum Singida alizungumza na ‘Single Mothers’ na kuwapatia historia yake kwa ufupi lengo likiwa ni kuwezeshana na kutiana moyo kwenye kila changamoto ambazo mama hupitia kuilea familia yake akiwa mwenyewe.


Chanzo - MuungwanaBlog

No comments:

Post a Comment