Monday, 18 December 2017

ZITTO KABWE ATAKA RAIS ZUMA AONDOLEWE MADARAKANI

 

Mbunge wa Kigoma mjini na kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma aondolewe kwenye nafasi ya Urais mara moja hata wiki hii.

Zitto Kabwe amesema hayo kupitia mtandao wake wa kijamii kufuatia uchaguzi wa Chama Cha ANC cha nchini Afrika Kusini ambapo walikuwa wakifanya uchaguzi kuchagua Rais na Makamu wake ndani ya chama.

"Jumatatu (leo) tutakuwa na Rais mpya wa Chama cha ANC. Kura zinapigwa hivi sasa huko Johannesburg. Ingawa nina ukakasi na Cyril Ramaphosa kuhusu Marikana, ninaunga mkono yeye kushinda na Makamu wake awe Lindiwe Sisulu. Pia Zuma aondolewe Urais mara moja baada ya wiki inayoanza kesho (leo)" aliandika Zitto Kabwe

Aidha Zitto Kabwe amesema kuwa ushindani wa uchaguzi wa ANC ni funzo kubwa kwa vyama vya siasa kuhusu Demokrasia ya ndani ya vyama hivyo.

"Uongozi imara wa Afrika Kusini ni muhimu sana kwa SADC na AU. Ushindani mkali wa Uchaguzi wa ANC ni funzo kubwa kwa vyama vyetu kuhusu Demokrasia ya ndani" aliandika Zitto Kabwe.


Chanzo - MuungwanaBlog

No comments:

Post a Comment