Friday, 15 September 2017

ZIDANE AMVULIA KOFIA RONALDO

Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane

KOCHA wa Real Madrid, Zinedine Zidane amesema kuwa mshambuliaji wa timu hiyo, Cristiano Ronaldo ndiye bora zaidi duniani kwa sasa.

Zidane ameyasema hayo muda mchache baada ya Ronaldo kufanikiwa kufunga mabao mawili kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya APOEL juzi.

Madrid ilifanikiwa kuibuka na ushindi huo, huku bao lingine la timu hiyo likiwekwa kiamini na beki na nahodha wa timu hiyo, Sergio Ramos.

Ronaldo alionekana kuwa na kasi ya juu kwenye Ligi ya Mabigwa Ulaya, kutokana na kuwa nje kwenye mechi zote za Ligi Kuu Hispania kutokana na kutumikia adhabu ya kukosa michezo mitano baada ya kumsukuma mwamuzi.

“Alikuwa anaweza kufunga mabao hata manne kama leo (juzi) angekuwa na bahati, kwangu huyu ni mchezaji bora wa dunia kwa sasa,” alisema Zidane mchezaji wa zamani wa Madrid.

Pamoja na kufunga mabao hayo, Real bado ilikuwa inaweza kushinda kwa mabao mengi kutokana na Ronaldo kugongesha mwamba na wakakosa nafasi kadhaa za wazi.

Pia Isco na Gareth Bale walikosa nafasi kadhaa za kufunga kwenye mchezo huo.


Chanzo - MuungwanaBlog

No comments:

Post a Comment