Friday, 15 September 2017

WAWILI WAUAWA MAJIBIZANO YA RISASI

Image result for Mkoa wa Ruvuma Gemini Mushi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Gemini Mushi

Watu wawili wamefariki dunia katika majibizano ya risasi kati ya polisi na watu hao katika kijiji cha Nangurukuru, kata ya Mandembo Tarafa ya Nampungu Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Gemini Mushi, polisi hao wakiwa katika majukumu mbalimbali ya ulinzi wa raia usiku wa kuamkia jana katika kijiji cha Nangurukuru walikutana na watu wakiwa kwenye pikipiki walijaribu kuwasimamisha walikaidi amri na kuanza kurusha risasi.

Kamanda Mushi amesema kuwa polisi kwa kutumia mbinu za medani walifanikiwa kuwashinda watu na hao na kuwapiga risasi na kufa papo hapo, ambapo walikutwa na bunduki aina SR pamoja na risasi 41 zinazotumiaka na silaha hiyo.

Katika Tukio jingine Jeshi la Polisi Wilaya ya Mbinga linamtafuta binti mmoja mwenye umri wa miaka 16 ambae jina lake limehifadhiwa kwa kosa la kutaka kumfukia mtoto wake mchanga anaekadiriwa kuwa na umri wa siku moja.


Chanzo -MuungwanaBlog

No comments:

Post a Comment