Friday, 15 September 2017

MAJAMBAZI WATATU WAUAWA DAR


Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm mnamo tarehe 13/09/2017 majira ya 21:00hrs huko maeneo ya kwa Mbiku Chamazi lilifanikiwa kukamata silaha moja bastola aina ya BERRETA yenye namba A065775Z ikiwa na risasi tano ndani ya magazine katika majibizano ya risasi kati ya askari polisi na majambazi wapatao watano(05).

Silaha hiyo ilipatikana baada askari kupata taarifa ya kuwepo kwa njama za majambazi hao watano (05) kufanya uporaji katika maduka ya M-Pesa/Tigopesa eneo hilo, na hatimaye kuweka mtego ambapo askari walifanikiwa kuwaona majambazi hao wakishuka kwenye gari yao kwa ajili ya kufanya tukio hilo.

Aidha baada ya majambazi hao kufika eneo la tukio na kugundua kuwa wanafuatiliwa na askari walianza kufyatua risasi kuwashambulia askari na ndipo askari walijibu mashambulizi na kufanikiwa kuwajeruhi majambazi watatu kati ya watano huku wengine wawili wakikimbia.

Silaha hiyo ilipopekuliwa kati ya risasi tano zilizokuwa ndani ya magazine moja ilikuwa chemba tayari kwa kutoka huku maganda sita ya silaha hiyo(pistol) yakipatikana eneo la tukio.

Majambazi waliojeruhiwa walifariki dunia baada ya kufikishwa hospitali ya taifa Muhimbili ili kupatiwa matibabu, Msako mkali unaendelea kuwatafuta majambazi wawili  waliokimbia.


Chanzo - MuungwanaBlog

No comments:

Post a Comment