Friday, 22 September 2017

KOCHA WA NJOMBE MJI: NILITISHIWA MAISHA


Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Njombe Mji, Hassan Banyai amezitaja sababu mbili zilizomfanya aamue kuachana na timu hiyo.


Banyai amesema sababu ya kwanza ni kutishiwa maisha na watu waliokuwa wanamuambia aawaachie timu yao.

“Lakini kulikuwa na viongozi pia wanaingilia kazi zangu, unapanga kikosi hiki, wao wanakuja wanalazimisha mchezaji fulani lazima acheze.

“Hakukuwa na utaratibu mzuri na kuheshimu taaluma, badala yake kila mtu anajua ukocha,” alisema.

Uongozi wa Njombe Mji, ulipokea barua yake ya kujiuzulu na kumtakia kila la kheri na sasa aliyekuwa msaidizi wake, Mrage Kabange ndiye anayeshikilia nafasi hiyo.


Chanzo - MuungwanaBlog

No comments:

Post a Comment