Friday, 22 September 2017

JAMBAZI MMOJA AULIWA NA POLISI


Jeshi la polisi Mkoa wa Songwe limewakabili watu wanne wanaosadikika kuwa majambazi wenye niaya kutekeleza tukio la uhalifu nyumbani kwa mfanyabiashara mkazi wa mji wa Viwawa wilayani Mbozi, ambapo katika majibizano ya risasi mtu mmoja amefariki.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe  (RPC) Mathius Nyange amesema baada ya kumpekua jambazi huyo wamemkuta na silaha tatu ikiwemo bunduki na risasi 3, upanga na kifaa cha kisasa kinachotumika kumzimisha mtu fahamu wakati wa kufanya tukio, hata hivyo jambazi huyo amefariki dunia kutokana na majeraha ya risasi.

Kufuatia tukio hilo wakazi wa mkoa wa Songwe wameshauri jeshi la polisi kuhakikisha usalama wa raia wanaothubutu kutoa taarifa kwa jeshi la polisi zinazohusu wahalifu na kusisitiza elimu ya polisi jamii na ulinzi shirikishi uimarishwe ili wananchi washiriki ipasavyo kutokomeza matukio ya uhalifu.

Aidha kamanda Nyange amesema mkoa wa Songwe sio mahali salama kwa watu wanofanya uhalifu na kuongeza kuwa wakija hawatarudi salama.


Chanzo - MuungwaBlog

No comments:

Post a Comment