Friday, 15 September 2017

DEREVA WA MBUNGE HECHE AKATWA MAPANGA NA WATU WASIOJULIKANA


Dereva wa Mbunge John Heche amevamiwa usiku wa kuamkia leo na watu wasiojulikana na kukatwa mapanga Mjini Tarime majira ya saa 2 usiku na hali yake siyo nzuri.

Mbunge John Heche amethibitisha kutokea kwa tukio hilo kutokana na taarifa alizopata kupitia Katibu wake, Mrimi Zablon ambaye amekiri Dereva huyo anayefahamika kwa jina la Suez Daniel Maradufu ni kweli amepata shambulio hilo na sasa yupo hospitali akipatiwa matibabu.

Kwa upande wa Kamanda wa Polisi Tarime Rorya, SACP Henry Mwaibambe alipotafutwa kwa njia ya simu na Mwandishi wetu amesema yupo kwenye kikao na akimaliza atatoa ripoti kamili.

Dereva huyo amelazwa katika hospitali ya Bomani Tarime mkoani Mara.

Chanzo - MuungwanaBlog

No comments:

Post a Comment