Saturday, 19 August 2017

MWENDESHA BODABODA AFA NA ABIRIA WAKE


WATU wawili wa kijiji cha Mitwana kilichopo katika kata ya Lukumbule Wilayani Tunduru, mkoani Ruvuma, wamefariki dunia katika ajali mbaya ya kugongana pikipiki na gari.


Ajali hiyo ilitokea katika kijiji cha Chailongo kilichopo katika Kata ya Mchesi na chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi waliokuwa wakiendesha vyombo hivyo.

 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Kamishina Mwandamizi wa Polisi Jemini Mushi, alimtaja mmoja wa waliopoteza maisha kuwa ni Husein Sollo, aliyekuwa akiendesha pikipiki yenye namba za usajiri MC 809 AUR.

Kamanda alimtaja mtu mwingine aliyekufa kuwa ni Athumani Tumu, ambaye alikuwa abiria wa pikipiki hiyo.

Kamanda  Mushi alisema kuwa katika tukio hilo, pikipiki hiyo iligongana uso kwa uso na gari aina ya Toyota Land Cruiser yenye namba za usajiri SM 4993 mali ya Hospitali ya Serikali ya Wilaya ya Tunduru.

 Alisema katika tukio hilo, gari hilo ambalo linadaiwa kuwa lilikuwa katika matengenezo, lilikuwa likiendeshwa na fundi aliyetambulika kwa jina la Michael Milinga ambaye anashikiliwa na polisi.

Kamanda alisema mtuhumiwa huyo atapelekwa mahakamani baada ya kukamilika kwa taratibu za uchunguzi na kuandika maelezo.


Chanzo - MuungwanaBlog

No comments:

Post a Comment