Wednesday, 4 January 2017

WASICHANA NA WAVULANA WAPEWE ELIMU YA AFYA YA UZAZI

Na Mwandishi wetu Nikolaus Paul Lyankando, TABORA

Imeelezwa kuwa washichana na wavulana wakipewa elimu ya afya ya uzazi na madhara ya mimba za utotoni watajiepusha na masuala ya ngono katika umri mdogo.

Hayo yamelisemwa jana na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mwalimu Queen Mlozi wakati akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake.

Alisema, kwa kutambua umuhimu wa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana serikali inashirikiana na mashirika ya kiraia kutoa elimu hiyo kupitia makongamano na matamasha ili kufikisha ujumbe.

Kwa upande wake Ofisa Mahusiano wa mradi wa Maries Stopes Bi. Symphrose Makungu alisema, vijana wa mkoa wa Tabora watapewa elimu hiyo ili kukabiliana na mimba na ndoa za utotoni.

Naye Mratibu wa afya ya uzazi, baba, mama na mtoto mkoa wa Tabora Marcelina Mpandachalo alibainisha kuwa, idadi ya wananchi wanaopata huduma ya uzazi wa mpango imeongezeka.

No comments:

Post a Comment