Monday, 16 January 2017

WADAU WA ELIMU: SERIKALI ICHUKUE HATUA KALI DHIDI YA WABADHIRIFU WA MALI ZA UMMA

NA PAUL KAYANDA-KAHAMA
WADAU wa Elimu katika Halmashauri ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga wameiomba  serikali  kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote waliohusika na ubadhirifu  wa bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Mwendakulima.
 
Wakizungumza kwa nyakati tofauti mjini Kahama wadau hao ambao hawakupenda majina yao yatajwe
Wamesema kuwa serikali iwachukulie hatua kali wale wote waliohusika  na  ubadhilifu  huo kufuatia tukio ambalo lingeweza kusababisha  vifo watoto wengi,iwapo  moto huo ugelipuka  nyakati  za  usiku wakiwa wamelala.
 
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya mji wa Kahama,  Anderson Msumba  akiongea na  vyombo vya Habari ofisini kwake amesema Halmashauri  yake tayari imetoa kiasi cha sh. milioni 10 pamoja na kuwanunulia vifaa mbalimbali vya mahitaji ya shule kwa wanafunzi waliothirika na  janga la moto kutokana na vitu vyao kuteketea  wakati wa tukio hilo.
 
Msumba amesema wiki iliyopita moto huo uliteketeza  bweni la wanafunzi wanaosoma kidato cha tano na sita  katika shule ya Sekondari Mwendakulima  na uliteketeza vitu vyote vya vya masomo  ya watoto hao majira ya saa nne na nusu asubuhi wakati wakiwa  mapumziko.
 
Aidha Msumba alifafanua kuwa kutokana na janga hilo lililowakumba Wanafunzi hao,mgodi wa Dhahabu Buzwagi uliopo Kata ya Mwendakulima  jilani zaidi na shule,msaada uliotoa ni pamoja na shuka 35 za kujifunika  usiku  pamoja na shuka 50 za kutandika waathirika  hao ambazo hakutaja thamani yake..

Akizungumzia  ubora wa bweni hilo amesema  Madiwani wa Halmashauri ya mji huo, walishawahi kulilalamikia  kuwa limejengwa chini ya kiwango sambamba na kuwa na  miundombinu mibovu ya umeme kwamba  lilijengwa kwa ghalama kubwa ya shilingi Mil. 200  zilizokuwa zimepingwa.

No comments:

Post a Comment