Wednesday, 4 January 2017

VIONGOZI WATUPIANA MPIRA UBEBAJI TAKA MTAA WA SKANDA

Image result for Picha za gari la taka
Picha ya Mtandao


NA NIKOLAUS PAUL LYANKANDO, TABORA

Diwani wa kata ya Mwinyi Mjini Tabora, Martin Mussa amesema yeye sio msemaji wa malalamiko ya wakazi wa mtaa Skanda katika kata hiyo wanaodai kutoliona gari la kubeba taka kama walivyokubaliana.

Akizungumza kwa njia ya simu Diwani huyo amesema, kiprotokali suala la mkandarasi wa tenda ya kubeba taka katika mtaa huo ni la mweyekiti wa mtaa.

Akihojiwa kwa njia ya simu mwenyekiti wa mtaa wa Skanda Bw. Maulid Moka amesema tatizo ni gari la mkandarasi.

"Tulikuwa na makubaliano na mkandarasi wa kuzoa taka ambaye alifanya kazi kwa wiki moja baada ya hapo makubaliano yetu yalikuwa aanze tarehe moja mwezi wa kumi na mbili lakini ilipofika tarehe moja tuliona kimya na nikampigia simu. Na hii haikuwa kandarasi ya mtaa wangu tu ilikuwa ni kandarasi ya kata nzima. Kwa hiyo nilipompigia simu aliniambia gari lake kwa mara ya mwisho lilipeleka tripu dampo lilivyofika kule likazama na baada ya kuondolewa likawa limepata hitilafu kwa hiyo likarudishwa gereji na kwa sasa hivi hana gari na akatuahidi kwamba atatuambia kinacho endelea lakin mpaka sasa hajatuambia, kwa hiyo na sisi tunashindwa kuwaambia wananchi wafanye nini". Amesema mwenyekiti

Hata hivyo, katika hali ya kushangaza mwenyekiti huyo wa mtaa wa Skanda ameonyesha kukerwa na kitendo cha kupigiwa simu na Divine FM ili kuhojiwa kuhusu gari la kubeba taka kwenye mtaa wake huku akimsisitiza mwandishi kama akitaka taarifa yoyote amtafute kazini kwake.

No comments:

Post a Comment