Wednesday, 4 January 2017

MWANAUME MMOJA AUA MKE NA MTOTO TABORA


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Khamis Selemani
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamisi Selemani

Na NIKOLAUS PAUL LYANKANDO, NZEGA - TABORA
Mwanaume mmoja amemuua mke wake kwa kumchoma kisu tumboni na kisha kumuua mwanawe mwenye umri wa miezi minne kwa kumnyonga.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Hamisi Selemani amesema kuwa tukio hilo limetokea huko Bukene Wilaya ya Nzega.

ACP Hamisi Selemani amesema, baada ya mtuhumiwa huyo kufanya tukio hilo alijaribu kujitoa uhai wake kwa kujichoma kisu na kukata sehemu zake za siri bila mafanikio na walifanikiwa kumkamata na kwamba mpaka sasa anaendelea na matibabu huku akiwa chini ya ulinzi mkali wa Polisi.

Aidha, Kamanda Hamisi Selemani ameiasa jamii kutatua migogoro yao ya kifamilia kwa njia za amani.

No comments:

Post a Comment