Wednesday, 4 January 2017

BINTI WA MIAKA 14 NA MWANAMKE WA MIAKA 40 WAUAWA HUKO TABORA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Khamis Selemani
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamisi Selemani

NA NIKOLAUS PAUL LYANKANDO, TABORA
Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 14 pamona ja mwanamke mwenye umri wa miaka 40 wameuawa katika matukio mawili tofauti katika wilaya za Igunga na Kaliiua Mkoani Tabora.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Kamishina Mzaidizi, Hamisi Selemani amesema tukio la kwanza limetokea katika kijiji cha Mbagala Wilayani Igunga ambapo mwanafunzi wa kike Nchambi Ng'wandu ameuawa kwa kupigwa na kipande cha mti kwenye paji la uso.

"Hili ni tukio ambalo tunaliita mauaji lakini ni tukio ambalo linahusisha watoto ambao waliku wanacheza na katika michezo yao imetokea mmoja akawa amefariki. Kwa hali kama hiyo sisi hatuwezi tukaliacha hivihivi tu, na matokeo yake kwa usalama wa mtoto ambaye amemuua mwenziye ingawa ni mtoto mdogo, kwa hiyo sisi tumemuhifadhi kituo cha polisi kwa ajili ya taratibu zingine. Hatuwezi tukamuacha hivihivi kwa usalama wake inaweza ikawa shida. Na hili tukio limetokea wialaya ya Igunga Mkoani Tabora". Amesema Kamanda Hamisi Selemani.

Akizungumzia tukio la pili amesema, mwanamke mmoja Kamwa Jilala mkazi wa Iyombo kata ya Kashishi, tarafa ya Ulyankulu wilayani Kaliua, ameuawa kwa kukatwa na mapanga.

"Kuna mama mmoja ni mkazi wa Ulyankulu ameuawa kwa kukatwa mapanga kichwani na sehemu mbalimbali za mwili wake na mtu asiyefahamika kwa jina ambaye alimvizia mama huyu akiwa melala nyumbani kwake na kumshambulia na baada ya mama huyo kushambuliwa majeraha ndiyo yalipelekea kifo chake. Hata hivyo kuna mtu ambaye tumemkamata, anafahamika na upelelezi bado unaendelea kuhusiana na tukio hili". Amesema Kamanda Hamisi Selemani.

Aidha, Kamishna msaidizi Hamisi Selemani ameeleza kuwa uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha mauaji ya mwanamke huyo ni mgogoro wa mashamba.

No comments:

Post a Comment