Monday, 18 December 2017

MKUTANO MKUU WA CCMA WAANZA LEO

Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) uliobeba ajenda kuu ya kukamilisha uchaguzi wa ndani wa chama hicho unaanza leo bila kuwa na shamrashamra zilizozoeleka katika mikutano iliyopita.

ZITTO KABWE ATAKA RAIS ZUMA AONDOLEWE MADARAKANI

 

Mbunge wa Kigoma mjini na kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma aondolewe kwenye nafasi ya Urais mara moja hata wiki hii.

TRUMP AKANUSHA KUTAKA KUMFUKUZA KAZI MWENDESHA MASHTAKA

 
Rais wa Marekani Donald Trump amekanusha tuhuma kwamba anampango kumfukuza kazi mwendesha mashtaka maalum wa nchi hiyo, Robert Mueller ambaye amekuwa akiongoza uchunguzi kuhusu tuhuma za Urusi kuingilia uchaguzi wa nchi hiyo.

Wednesday, 11 October 2017

MVUA YALETA MAAFA RUKWA


KAYA 11 zimebaki bila makazi baada ya mvua kubwa kunyesha na kuezua nyumba katika kijiji cha Matai Asilia, wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa.

MIAKA 30 JELA KWA WIZI WA KUTUMIA NGUVU


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imewahukumu watu wanne kwenda jela miaka 30 kila mmoja na kuchapwa viboko 12 baada ya kupatikana na hatia ya unyang'anyi wa mali ya zaidi ya Sh. milioni mbili.

CHADEMA YAPATA PIGO JINGINE


Chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa kimeendelea kujiimarisha kwa kuvuna wanachama watano kutoka chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) manispaa ya Iringa wakiwa na mikakati ya kuja kulikomboa jimbo la Iringa mjini ambalo lipo chini ya chama cha CHADEMA.

NDEGE ZA KIVITA ZA MAREKANI ZAPAA RASI YA KOREA


Ndege hizo za kuangusha mabomu zilipaa kutoka kisiwa cha Marekani cha Guam

Marekani kwa mara nyingine imefanya mazoezi ya kijeshi kwa pamoja na Korea Kusini, ambapo ndege zake mbili za kivita za kuangusha mabomu zimepaa juu ya rasi ya Korea.

KATIBU MWENEZI BAVICHA APATA AJALI


Katibu Mwenezi wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha), Edward Simbeye amepata ajali ya gari.

Saturday, 23 September 2017

KESI YA OKWI YAIWEKA PABAYA YANGAKasi ya mabao ya mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi, imeiweka Yanga katika wakati mgumu kwani hata wakishinda dhidi ya Ndanda FC leo Jumamosi, hawawezi kupanda na kuwa juu ya Simba ambayo imeapa kuondoka na taji msimu huu.

TRUMP NA RAIS WA KOREA KASKAZINI WAFIKIA PABAYA, WAITANA "WENDAWAZIMU"

Raisi Kim Jong Un na mwenzanke Donald Trump

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amesema kuwa matamshi ya rais wa Marekani Donald Trump aliyemtaja kuwa ''na matatizo ya kiakili'' yamempatia motisha zaidi ya kuendelea kutengeza makombora ya taifa lake.

RAIS MAGUFULI ATOA KAMISHENI 422


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa nchi Dkt. John Pombe Magufuli, leo amewatunuku kamisheni maafisa wa Jeshi 422 ambao wamehitimu mafunzo mbali mbali kwenye chuo cha Jeshi Monduli mkoani Arusha.

MAGUFULI KUMWAGA AJIRA 3,000

Rais John Pombe Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa nchi Dkt. John Pombe Magufuli, ametangaza kutoa ajira kwa wanajeshi 3000 wapya mwaka huu, ili jeshi la Tanzania liweze kuwa na askari wa kutosha.

Friday, 22 September 2017

IBADA YA JUMAPILI SEPTEMBER 10, 2017 - CGRA KAHAMA (GEREZA KUU LA MAISHA YAKO)

Bwana Yesu Asifiwe mwana wa Mungu, Ninakusalimu katika Jina kuu la Yesu. Karibu tuweze kushiriki kwa kusikiliza Ibada iliyofanyika katika Kanisa la Christian Gospel Revival Assembly (CGRA) Tarehe 10/09/2017. Ibada hii ilikuwa na somo lililohusu GEREZA KUU LA MAISHA YAKO ambalo lilifundishwa na MTU WA MUNGU BISHOP JOVIN MWEMEZI.


Karibu sana na Ubarikiwe!!!

RC MONGELA ASHANGAZWA GARI KUKOSA DEREVA MWAKA MZIMA


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella ameonyesha kusikitishwa kwa kutotumika kwa gari ya wagonjwa uliofanywa na viongozi wa halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe ambao wameshindwa kutumia gari hiyo kwaajiri ya kubeba wagonjwa jambo ambalo anasema kuwa kama Rais Magufuli akijua wataonekana ni watu wa ajabu.

JAMBAZI MMOJA AULIWA NA POLISI


Jeshi la polisi Mkoa wa Songwe limewakabili watu wanne wanaosadikika kuwa majambazi wenye niaya kutekeleza tukio la uhalifu nyumbani kwa mfanyabiashara mkazi wa mji wa Viwawa wilayani Mbozi, ambapo katika majibizano ya risasi mtu mmoja amefariki.

KOCHA WA NJOMBE MJI: NILITISHIWA MAISHA


Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Njombe Mji, Hassan Banyai amezitaja sababu mbili zilizomfanya aamue kuachana na timu hiyo.

MWANAMKE TAJIRI ZAIDI DUNIANI AFARIKI


Bi Bettencourt alikuwa mtu wa 14 katika orodha ya watu tajiri zaidi duniani, kulingana orodha ya jarida la Forbes ya mwaka 2017

TUME YASOGEZA UCHAGUZI MBELE

Mwenyekiti wa Tume ya IBEC, Wafula Chebukati

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya (IEBC), imebadilisha tarehe ya kufanyika uchaguzi wa marudio na kwamba badala ya Octoba 17 sasa utafanyika Oktoba 26.

WANASAYANSI WATENGENEZA KINGA INAYOWEZA KUSHAMBULIA HIV KWA 99%


Wanasayansi wamekuwa wakitengeneza chembe chembe za kinga ya mwili zinazoweza kushambulia asilimia 99% ya virusi vya HIV vinavyosababisha ukimwi na hivyo kuzuwia maambukizi kuendelea.

Monday, 18 September 2017

MOURINHO KUMREJESHA ROONEY MANCHESTER UNITED?


Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amesema anaamini ipo siku nyota wa zamani wa timu hiyo Wayne Rooney atarejea klabuni hapo.

WANAFUNZI 16,000 HATARINI KUKOSA MIKOPO YA ELIMU YA JUU


WAKATI mwezi mmoja umebaki kabla ya mwaka mpya wa masomo kuanza kwa vyuo vikuu nchini, Wanafunzi wa elimu ya juu wapatao 16,000 kati ya 61,000 walioomba kupata mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) wako hatarini kuikosa hata kabla ya zoezi hilo kuanza kutokana na taarifa za maombi yao kuwa na dosari.

WALIMU 3,000 WAKOSA VIGEZO


SERIKALI imesema jumla ya walimu 2,939 sawa na asilimia 19.5 walioomba kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya astashahada na stashahada kwa mwaka wa masomo 2017/18, wamebainika kutokuwa na sifa zinazotakiwa kujiunga na mafunzo hayo.

ASKARI POLISI WAWILI WAHUKUMIWA MIAKA 35 JELA


Mahakama Kuu ya Tanzania imewahukumu askari Polisi wawili wa kutoka kituo cha Oysterbay jijini Dar es Salaam na watu wengine sita kwenda jela miaka 35 kwa makosa mawili ya kukutwa nyara za serikali na kujihusisha na mtandao wa ujangili.

TANZANIA YASAMEHEWA DENI LA BILIONI 445 NA BRAZIL


Serikali ya Brazil imeisamehe Tanzania deni Dola 203milioni ambazo sawa Bilioni 445 ambalo limetokana na mkopo uliotolewa kwaajili ya ujenzi wa barabara ya Morogoro-Dodoma mwaka 1979.

KIMBUNGA KIKALI CHAUA WATU 8


Kimbunga kikali na chenye nguvu kubwa kimetokea magharibi mwa Romania na kuuwa watu wanane pia kujeruhi wengine zaidi ya 67, kwa mujibu mwa maafisa wa eneo hilo.

MAREKANI YATATHMINI KUFUNGA UBALOZI WAKE CUBA


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson amesema Washington inathamini iwapo ifunge ubalozi wake nchini Cuba, baada ya kutokea mlolongo wa mashambulizi ya kelele kwa wafanyakazi wake.

Friday, 15 September 2017

KIJANA AUAWA UBONGO WAKE WATOLEWA


Kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 17 ambaye ana ulemavu wa ngozi amekutwa akiwa ameuawa na ubongo wake kutolewa  huko nchini Msumbiji.

SERIKALI YAWAKOMALIA MAKAHABA


Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto kwa ushirikiana na Wizara ya Mambo ya ndani, na Ofisi ya rais TAMISEMI imesema itahikikisha Wanawake wanaojihusisha na biashara ya ukahaba wanaendelea kukamatwa ili kulinda hadhi ya mwanamke.

TANZANIA YASHANGAZWA NA UCHUNGUZI WA UN KUHUSU KOREA YA KASKAZINI

Dr Augustine Mahiga,Waziri wa Mambo ya Nje, Tanzania
Dk. Augustine Mahiga, Waziri wa mambo ya nje, Tanzania
Tanzania imesema imeshtushwa baada ya kuorodheshwa miongoni mwa nchi ambazo zimechunguzwa na Umoja wa Mataifa na kuhusishwa kuwa na uhusiano wa kibiashara na Korea Kaskazini.

NDUGAI AWAASA WABUNGE KUTOKAA BAA


Spika Ndugai leo amewausia wabunge wanzake kuwa makini na usalama wao kwa kuchukua hatua zaidi za kujilinda, ikiwemo kutokaa baa mpaka usiku wa manane ili kujiepusha na matatizo mbali mbali yatakayoathiri usalama wao.

UMESIKIA MABADILIKO YA KOMBE LA DUNIA?


Shirikisho la soka la kimataifa FIFA limebadili utaratibu wa namna ya kupanga makundi katika fainali za Kombe la dunia 2018 nchini Urusi.

MAJAMBAZI WATATU WAUAWA DAR


Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm mnamo tarehe 13/09/2017 majira ya 21:00hrs huko maeneo ya kwa Mbiku Chamazi lilifanikiwa kukamata silaha moja bastola aina ya BERRETA yenye namba A065775Z ikiwa na risasi tano ndani ya magazine katika majibizano ya risasi kati ya askari polisi na majambazi wapatao watano(05).

BREAKING NEWS: MAHAKAMA YAMFUTIA KESI GWAJIMA


KISUTU: Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amefutiwa kesi ya kushindwa kutunza silaha baada ya mahakama kushindwa kuthibitisha mashtaka hayo, na kuamuru arudishiwe mkoba wenye silaha yake.

Chanzo - MuungwanaBlog

ZIDANE AMVULIA KOFIA RONALDO

Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane

KOCHA wa Real Madrid, Zinedine Zidane amesema kuwa mshambuliaji wa timu hiyo, Cristiano Ronaldo ndiye bora zaidi duniani kwa sasa.

RC RUKWA: "NATAKA TUWACHOME WAHALIFU"

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Kamishna mstaafu Zelote Stephen (Aliyevalia kaunda suti).

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amefunguka na kudai kukamata na kuchoma nyavu kwa wavuvi haramu haitoshi bali wanapaswa wakamatwe na wachomwe wahalifu hao kwa kutumia sheria ili vitendo hivyo visiweze kujirudia.

WALIONASWA NA SHEHENA YA ALMASI WAFIKISHWA KORTINI


WATUHUMIWA waliokamatwa na mzigo wa Almasi zenye thamani ya Sh 32.3 bilioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA), wamefikishwa Mahakamani Kisutu asubuhi leo Ijumaa.

WAWILI WAUAWA MAJIBIZANO YA RISASI

Image result for Mkoa wa Ruvuma Gemini Mushi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Gemini Mushi

Watu wawili wamefariki dunia katika majibizano ya risasi kati ya polisi na watu hao katika kijiji cha Nangurukuru, kata ya Mandembo Tarafa ya Nampungu Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma

GEITA HAPATOSHI


Geita. Madiwani wawili kuwekwa rumande na kuvunjwa kioo cha gari la halmashauri ni miongoni mwa matukio yaliyotikisa mjini Geita, polisi walipowadhibiti wawakilishi hao wa wananchi waliofunga barabara kushinikiza malimbikizo ya malipo ya ushuru.

CCM WAMPONGEZAMBUNGE WAO WA CCM ALIYEKODI NDEGE YA KUMSAFIRISHA TUNDU LISSUChama Cha Mapinduzi (CCM) kimempongeza mwanachama wake aliyejitolea kudhamini ndege iliyomsafirisha Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu kwenda jijini Nairobi nchini Kenya kwaajili ya matibabu.

ATCL YAPUNGUZA HASARA KWA BILIONI 17/-

Mkurugenzi mkuu ATCL, Ladislaus Matindi

KAMPUNI ya Ndege Tanzania (ATCL), imepunguza hasara kwa kiasi kikubwa kutoka Sh bilioni 20 hadi kufi kia Sh bilioni 3 kwa mwaka.

KOREA KASKAZINI YAFANYA JARIBIO, LAPITIA JAPAN


Korea Kaskazini imefanya jaribio jingine la kombora lililopita kwenye anga ya Japan Alhamisi Septemba 14 saa nne usiku saa za kimataifa (sawa na Ijumaa asubuhi Septemba 15 saa za Tokyo). Kombora hilo lilirushwa kupitia kisiwa cha Japan cha Hokkaido, kwa mara ya pili katika muda wa wiki tatu.

DEREVA WA MBUNGE HECHE AKATWA MAPANGA NA WATU WASIOJULIKANA


Dereva wa Mbunge John Heche amevamiwa usiku wa kuamkia leo na watu wasiojulikana na kukatwa mapanga Mjini Tarime majira ya saa 2 usiku na hali yake siyo nzuri.

Saturday, 26 August 2017

HATA MIMI SIWATAMBUI AKINA SEIF - NDUGAI


Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amefunguka na kusema hata yeye pia hawatambui CUF upande wa Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad kwa kuwa watu hao hawatambuliki kwa msajili wa vyama vya siasa nchini. 

NIYONZIMA - NIMETISHIWA KUUAWA

Kiungo wa kimataifa wa Klabu ya Simba Haruna Niyonzima.

Kiungo wa kimataifa wa Klabu ya Simba Haruna Niyonzima amefunguka na kudai haikuwa jambo rahisi yeye kuchukua maamuzi ya kuchezea Simba ila anamshukuru Mungu kwa kumtoa hofu ya kushambuliwa na kuuliwa na mashabiki wa Yanga wasiofahamu mchezo.

MKUU WA MKOA AKAMATA MADINI


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amekamata na kuzuia uuzwaji wa tani 2,143 za madini aina ya "Clinker" yanayotumika katika kuzalishia saruji kutokana na wingu la ubabaishaji uliogubika usafirishaji madini hayo kwenda nje ya nchi.